
Wakali wa namba kikapu Dar
SUPASTAA wa Christ The King, Davidson Evarist anawaburuza wenzake katika utupiaji nyavuni kwenye mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza Mkoa wa Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya Bandari, Kurasini. Davidson amegeuka kuwa tishio kutokana na namna anavyokabiliana na timu pinzani na pia wepesi wake katika kuzamisha mipira nyavuni hadi sasa akiwa amejikusanyia pointi 406….