
Mkutano wa nishati: JNICC kumeanza kuchangamka
Dar es Salaam. Mambo yameanza kuchangamka katika viunga vya kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), unakofanyika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati. Kabla ya ratiba rasmi ya wahudhuriaji kuingia ukumbini, tayari burudani mbalimbali zimeanza kushuhudiwa nje ya kituo hicho. Ngoma ya Msewe, yenye asili yake Unguja visiwani Zanzibar, ndiyo iliyofungua milango…