Ving’ora, vimulimuli janga barabarani | Mwananchi

Dar es Salaam. Januari 26-28, 2025 baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam yalikuwa kwenye mwonekano tofauti na ule uliozoeleka kwa muda mrefu. Barabara takribani tisa za kuingia katikati ya jiji zilifungwa kwa muda ndani ya siku sita huku ulinzi ukiimarishwa kila kona. Mabadiliko hayo yalilenga kuhakikisha  usalama na utulivu kwa wageni waliohudhuria…

Read More

DPP amkatia rufaa Dk Slaa Mahakama ya Rufani

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) amewasilisha kusudio la kukata rufaa kupinga uamuzi uliyotolewa jana na Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam dhidi ya Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania, Dk Wilbrod Slaa. Uamuzi wa Mahakama Kuu jana, ulielekeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kushughulikia suala la dhamana ya mwanasiasa huyo na kutoa…

Read More

Sarafu moja EAC yapigwa kalenda hadi hadi 2031

Dodoma. Mpango wa utekelezaji wa azimio la kuwa na sarafu moja ifikapo 2024 katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, umesogezwa mbele kwa miaka saba mingine na sasa mpango huo unatarajiwa kufikiwa 2031. Katika swali lake bungeni leo Januari 31, 2025, Mbunge wa Kinondoni (CCM) Abbas Tarimba ameuliza utekelezaji wa azimio la kuwa na sarafu moja ifikapo…

Read More

Aliyeongoza mapinduzi ya Rais Assad Syria apewa uongozi

Dar es Salaam. Kiongozi wa kundi la Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sham (HTS), Ahmed al-Sharaa ameteuliwa kuwa Rais wa mpito ya Syria, ikiwa ni takriban siku 53 zimepita tangu alipoongoza kuondolewa madarakani uongozi wa Bashar al-Assad. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Januari 30, 2025 na Kamanda Hassan Abdel Ghani, msemaji wa Kamandi ya Operesheni…

Read More

Trump atoa kauli mgogoro wa Rwanda, DR Congo

Dar es Salaam. Rais wa Marekani, Donald Trump amesema mgogoro kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) “ni tatizo kubwa sana.” Trump amebainisha hilo Alhamis Januari 30, 2025 akijibu swali la mwandishi aliyemuuliza kuhusu kinachoendelea baina ya Rwanda na DRC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu ajali ya ndege iliyotokea…

Read More

Lwasa anataka 10 tu ya kuanzia 

KIUNGO mshambuliaji wa Kagera Sugar, Peter Lwasa amesema anatamani mzunguko wa pili wa Ligi Kuu afunge mabao matano na kufikisha 10 msimu huu. Nyota huyo raia wa Uganda alisajiliwa na Kagera Sugar msimu huu akitokea KCCA ya nchini kwao alikodumu msimu mmoja. Tanzania inakuwa nchi ya nne kucheza soka baada ya Uganda (KCCA na URA),…

Read More