Rupia kidogo tu asepe Singida Black Stars

MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars, Mkenya Elvis Rupia amesema ilibaki kidogo tu aondoke dirisha dogo la usajili la Januari baada ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo japo kwa sasa kila kitu kipo freshi. Nyota huyo anayeongoza wafungaji mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na manane, alisema kuna mambo ambayo hapendi kuyaweka wazi yalitaka kumfanya aondoke….

Read More

Msigwa: Faida ya ATCL ni zaidi ya mapato ya shirika

Dar es Salaam. Serikali imewataka wananchi kutoangalia faida zinazopatikana kwa Shirika la ndege Tanzania (ATCL), kwa watu wanaokata tiketi peke yake, kwani linachangia kukuza sekta nyingine ikiwemo utalii. Hayo yamesemwa leo Jumamosi na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Hifadhi ya Mikumi, mkoani Morogoro. Msigwa amesema…

Read More

Mserbia KenGold bado tatu za nguvu

KOCHA wa KenGold, Mserbia Vladislav Heric, amesema anahitaji zaidi ya michezo mitatu ya nguvu ya kirafiki ili kujiweka fiti na mzunguko wa pili, huku akiomba viongozi kufanyia kazi suala hilo haraka kabla ya Ligi Kuu Bara kurejea Februari Mosi. Kauli ya kocha huyo inajiri baada ya kupata mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Maafande…

Read More

Wanne wakutwa na kipindupindu Mbeya, hatua zachukuliwa

Mbeya. Wakati Kata ya Isyesye jijini Mbeya ikitaja watu wanne kugundulika kuwa na kipindupindu, serikali ya kata hiyo imesema itawachukulia hatua kali wazazi na walezi watakaokaidi kulipia chakula cha wanafunzi shuleni ifikapo Januari 30 mwaka huu ili kuepusha kuenea kwa ugonjwa huo. Pia imekataza aina yoyote ya mikusanyiko na vyakula pale inapotokea msiba wa aina…

Read More

Marekani yaanza kuwafukuza wahamiaji, ndege za kijeshi zatumika

Washington. Ameanza! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Jeshi la Marekani kuanza utekelezaji wa amri iliyotolewa na Rais Donald Trump ya kuwarejesha kwao (deportation) wahamiaji haramu wanaoishi nchini. Televisheni ya ABC news imeripoti leo Jumamosi Januari 25, 2025, kuwa mamia ya wahamiaji wameonakena wakipandishwa kwenye ndege za kijeshi huku wakiwa wamefungwa pingu na minyororo tayari kurejeshwa…

Read More