
AKILI ZA KIJIWENI: Feruzi afuate nyayo za Dilunga
JAMBO lililotukosha hapa kijiweni ni kipa Feruzi Teru aliyekuwa chaguo la tano pale Simba kujiunga na Kagera Sugar dirisha dogo. Kilichotufurahisha ni mdogo wetu kupata ufahamu kuwa alikuwa anapoteza muda na kipaji chake pale Simba kwani nafasi ya kucheza isingekuwa rahisi kupatikana kwake. Fikiria bila kumhesabu Ayoub Lakred, Feruzi mbele yake kulikuwa na makipa wanne…