
Serikali yataja chanzo katikakatika umeme
Unguja. Wakati baadhi ya wananchi na wafanyabiashara kisiwani hapa wakilalamikia katikakatika ya umeme, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Shaib Hassan Kaduara, amesema inasababishwa na ongezeko la watumiaji na wawekezaji nchini. Hata hivyo, amesema Serikali inatarajia kuleta msongo mpya wa umeme wenye megawati 220 kutoka Tanzania Bara mapema mwaka huu. “Unaotumika sasa una megawati…