
KONA YA FYATU MFYATUZI: Rushwa, najifyatua, nafyatua, tufyatuane
Nachukia rushwa iwe ndogo, kubwa, ya fedha, ngono, vyeo, nk. Zaidi, nawachukia watoaji, wapokeaji, na wanene wanaojifanya kutoiona, hivyo, kutoifyatua. Japo hatuongelei waziwazi, rushwa ni kansa ya kaya. Hivyo, leo, najifyatua, nawafyatyua, na nahimiza tuwafyatue na kufyatuana ili kuikabili, kuifyatua, na kuiondosha rushwa. Japo rushwa hufanyika kisiri, tukifyatuka vilivyo na kuitangazia operesheni na vita kuifyatua…