
Faida, hasara minyukano ya vigogo Chadema
Dar es Salaam. Minyukano ya viongozi na wanachama wa Chadema wanaomuunga mkono Mwenyekiti wao Freeman Mbowe na wanaomuunga mkono Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, imetafsiriwa kwa sura mbili tofauti. Sura ya kwanza imetajwa kuwa mbaya inayolenga kukibomoa chama hicho, huku wengine wakiamini kuwa minyukano hiyo inathibitisha uwazi na kuwakumbusha viongozi kwamba hakuna siri…