Ahmed Ally ampa Chasambi ujumbe mzito

Meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amemtaka winga Ladack Chasambi asivurugwe na bao alilojifunga kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate, leo Februari 6, 2025. Winga huyo alijifunga bao hilo baada ya mpira mrefu aliourudisha kushindwa kuokolewa na kipa Moussa Camara na kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa bao 1-1. Ahmed Ally amesema kuwa…

Read More

Aunganishwa na kaka yake kesi ya kughushi wosia

Dar es Salaam. Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Nargis Omar(70) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili ya kughushi wasio wa mama yake. Nargis anadaiwa kughushi wosia wa marehemu mama yake mzazi kisha kujipatia nyumba kinyume cha sheria. Mshtakiwa huyo amefikishwa  mahakamani hapo leo, Alhamisi Februari 6, 2025 na kusomewa…

Read More

Wataalamu wafunguka ishu ya kadi Fountain gate vs Simba

KOCHA Fadlu Davids ameshindwa kuifikia rekodi ya Patrick Aussems ya kushinda mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu baada ya jioni ya jana kulazimishwa sare ya 1-1 na Fountain Gate iliyomaliza pungufu baada ya kipa John Noble kutolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi Abel William kutoka Arusha. Fadlu aliyetua Msimbazi msimu huu aliiongoza Simba kushinda mechi…

Read More

Jinsi siku 1000 zinavyomsaidia mtoto kumkinga na maradhi 13

Unguja. Iwapo wazazi watazingatia malezi kwa siku 1000 za kwanza zitasaidia kumkinga mtoto na maradhi 13 ikiwamo kupunguza vifo vya mama na mtoto kisiwani Zanzibar. Imeelezwa Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar, Dk Salim Slim ambapo amesema siku hizo ni muhimu kwa makuzi ya mtoto, lakini wazazi wengi wanazipuuzia hivyo kusababisha…

Read More

Dk Mpango awataka vijana kuwatunza, kuwathamini wazazi

Rombo. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amewataka vijana nchini waliobahatika kuwa na wazazi walio hai kujenga utamaduni wa kuwatunza, kuwalea na kuwaonyesha upendo. Amesema mzazi (mama) ni mtu muhimu kwa kuwa ndiye wakili wa Mwenyezi Mungu hapa duniani. Hayo ameyasema leo, Februari 6, 2025 wakati wa ibada ya misa ya mazishi ya  mama mzazi…

Read More

WATAFITI WASHAURIWA KUCHAPISHA MATOKEO YA TAFITI KWA KISWAHILI ILI KUFIKIA JAMII

Farida Mangube, Morogoro  Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Mussa Ali Mussa, amewataka watafiti kuchapisha tafiti zao kwa Kiswahili ili kuhakikisha matokeo ya utafiti yanafika kwa jamii inayolengwa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa utafiti wa magonjwa yanayo ambukizwa kutoka Kwa wanyama kwenda kwa binaadamu unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo…

Read More

Mawaziri washambulia hoja za kamati

Dodoma. Mawaziri wameshambulia kujibu hoja za wabunge, huku Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo akitaja mikakati ya kutatua changamoto ya ajali nchini. Hoja hizo zilitolewa na wabunge wakati wakiwasilisha na kuchangia taarifa za kamati za Kudumu za Viwanda, Biashara, Kilimo, Uvuvi na Mifugo na ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama…

Read More