
Wasira ataka vijana kutotumika Kisiasa akikitaja Chadema, Heche amjibu
Tarime. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amewataka vijana wilayani Tarime Mkoa wa Mara kuacha kutumika kisiasa kwa lengo la kusababisha fujo na machafuko ndani ya wilaya hiyo. Akizindua ofisi ya CCM Kata ya Nyakonga wilayani Tarime leo Jumapili Februari 9, 2025, Wasira amesema baadhi ya vijana wilayani humo wanatumika vibaya kwaajili…