Marekani Kusitisha Misaada Balaa Jipya DR Congo – Global Publishers



Hatua ya Rais Donald Trump ya kusitisha misaada yote iliyokuwa ikitolewa na Marekani imeongeza hali ya wasiwasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako mamilioni ya wakimbizi walikuwa wakitegemea misaada hiyo.

Afisa kutoka Umoja wa Mataifa, Bruno Lemarquis, amenukuliwa akisema kwamba DRC ilikuwa ikipokea asilimia 70 ya misaada ya kibinadamu kutoka Marekani. Uamuzi wa Trump umesababisha upungufu mkubwa wa mahitaji muhimu kwa wakimbizi.

Lemarquis ameongeza kuwa kwa mwaka 2024 pekee, DRC ilipokea dola milioni 910 kutoka Marekani pamoja na misaada mingine kwa waathirika wa mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi nchini humo.


Related Posts