Trump Aikandia Canada Kwa Kuitegemea Marekani – Global Publishers



Rais Donald Trump wa Marekani ameendelea kutoa kauli za dharau kwa mataifa kadhaa mara hii akiishambulia tena Canada akisema haifai kama nchi bila msaada wa kiuchumi na ulinzi wa kijeshi wa Marekani.

Kadhalika Trump amekariri pendekezo lake la kutaka Canada kujiunga na Marekani kama jimbo la 51, wazo ambalo serikali ya Canada inalipinga vikali.

Kwa mujibu wa Trump, kuafiki kuwa jimbo la 51 la Marekani litakuwa jambo kubwa zaidi ambalo [Canada] linaweza kufanya.
Tramp amedai kuwa, Canada hailigharamii sana jeshi lake, na hii inatokana na wao kudhani kwamba tutawalinda … hawalipi sehemu yao ya jeshi kwa NATO.

Trump ameendelea kusema: “Jambo jingine ni kwamba, tunawapa ruzuku ya kiasi cha dola bilioni 200 kwa mwaka. Ikiwa tutaacha kufanya hivyo, na ikiwa hatutawaruhusu kutengeneza magari kupitia ushuru na vitu vingine – magari, lori, n.k., (Canada) haifai kabisa kama nchi.”
Tangu aingie madarakani rasmi Januari 20, mwaka huu Trump amekuwa akiyatishia mataifa ya dunia kwa vikwazo, kukata misaada, na ushuru wa juu, zikiwemo hata nchi rafiki na Marekani.