Rais Donald Trump wa Marekani amezitaka balozi za nchi hiyo duniani kote kujiandaa kwa upunguzwaji mkubwa wa wafanyakazi ikiwa ni mwendelezo wa kupunguza mzigo wa serikali na kubadili mfumo wote wa Kidiplomasia wa Marekani.
Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya balozi zimepewa maelekezo ya kupunguza wafanyakazi ambao ni Wamarekani pamoja na wazawa wa nchi husika kwa mpaka asilimia 10 ambapo orodha ya wanaopaswa kupunguzwa inatakiwa kuwasilishwa leo, Februari 14, 2025.
Pia Serikali ya Marekani imesitisha mikataba na takribani wazabuni 60 waliokuwa wakitoa huduma mbalimbali kwenye balozi za Marekani duniani kote.