
Buidhaa hizi zapaisha mfumuko wa bei Zanzibar
Unguja. Mfumko wa bei kwa Januari 2025 Zanzibar umeongezeka na kufikia asilimia 5.27 kutoka asilimia 4.9 iliyorekodiwa Desemba 2024, huku bidhaa za mchele na ndizi zikichangia kwa kiwango kikubwa. Bidhaa zilizosababisha kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mchele wa mapembe kwa asilimia 1.5, mchele wa Mbeya asilimia 4.4, mchele wa Jasmin asilimia 0.8,…