Chebukati afariki dunia akiwa hospitali Nairobi

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya, Wafula Chebukati, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.

Taarifa kutoka kwa familia yake zinaeleza kuwa Chebukati alifariki jana Februari 20, 2025, katika hospitali moja jijini Nairobi alipokuwa akipatiwa matibabu.

Aidha, Chebukati ameugua kwa takriban wiki moja na alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kabla ya kufariki.

Chebukati alihudumu kama mwenyekiti wa IEBC kuanzia Januari 2017 hadi Januari 17, 2023, akisimamia chaguzi kuu za Kenya za mwaka 2017 na 2022.

Katika hotuba yake ya kuaga IEBC, alieleza kuridhika na kazi yake, akisema tume hiyo “ilipitia mawimbi makali yaliyotishia uhai wake, lakini ilidumu imara.”

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts