WAZIRI SILAA AZINDUA KAMPENI YA SITAPELIKI ARUSHA.

Na Pamela Mollel,Arusha

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh.Jerry Silaa amezindua kampeni maalum ijulikanayo kama “SITAPELIKI”yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujikinga na utapeli katika mitandao

Kampeni hiyo amezindua jijini Arusha katika kikao kazi cha serikali na wadau wa sekta ya mawasiliano na Teknolojia ya habari kuhusu utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa uchumi wa kidigitali 2024-2025

Waziri Silaa anasema kuwa watanzania wanatakiwa kufahamu w atoa huduma wote wa mawasiliano ambapo watatumia namba 100 katika kutoa huduma zao

Aidha ametaja mafanikio ya wizara hiyo kuwa ni pamoja na ufikishwaji wa mkongo wa Taifa katika wilaya 109 kati 139 nchini Sawa na asilimia 78

Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wizara ya ujenzi,mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Bi.Hawa Ibrahim anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Tanzania kuwa na uchumi wa kidigitali

Anaongeza kuwa wamekuwa wakipata misaada mikubwa katika sekta ya mawasiliano ambapo wamepata mradi ambao watajenga kituo cha ubunifu itakayosaidia kuweka vijana katika ulimwengu wa kidigitali.

 

Related Posts