Ujerumani Yatoa Onyo Dhidi Ya Marekani – Global Publishers



Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock amesema Ulaya haipaswi kusita kuweka shinikizo dhidi ya Marekani, iwapo nchi hiyo itashindwa kukumbatia demokrasia ya kiliberali.

Waziri Annalena ameyasema hayo kufuatia mazungumzo kati ya Marekani na Urusi ambayo yamewatenga wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya na Ukraine.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni huko Potsdam juzi mwanasiasa huyo wa Chama cha Kijani alisema, “Tunaongeza mashinikizo kwa Wamarekani ili wajue wana mengi ya kupoteza ikiwa hawatasimama upande wa demokrasia huria za Ulaya.

“Hakuna anayeweza kuamua kuhusu vita na amani kwa Waukraine au sisi Wazungu (watu wa Ulaya), na huu ndio msimamo wa Wajerumani,” amesisitiza Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Ujerumani.

Wachunguzi wa kiasa wanasema, kurejea kwa Rais Donald Trump katika Ikulu ya White House ya Marekani kumevuruga kabisa matarajio ya viongozi wa Ulaya kuhusu kumalizika kwa vita vya Ukraine.

Kadhalika Rais huyo wa Marekani hivi karibuni alimshambulia vikali Rais Vladimir Zelensky wa Ukraine, na kumtaja kama “dikteta asiyechaguliwa.”


Related Posts