Chalamila awaita vijana wasio na mitaji ofisini kwake

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema vijana wanaotaka kufanya biashara eneo la Kariakoo wafike ofisini kwake ili kukopeshwa bidhaa za kuanzia kama mtaji. Chalamila ameyasema hayo leo Alhamisi Februari  27, 2025 katika sherehe za kilele cha uzinduzi wa ufanyaji biashara saa 24,uliofanyika jijini humo. Shughuli za ufanyaji biashara…

Read More

BoT yaweka kibano mikopo ‘kausha damu’

Mtwara. Baada ya wabunge kucharuka kuhusu mikopo ‘kausha damu’ kwenye mitandao, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekuja na mwarobaini unaozuia mkopeshaji kuingia kwenye namba za simu za mteja. Mbali na hilo, BoT imeelekeza kampuni inayokopesha kwenye mtandao iweke wazi masharti yake na si kuandika ‘masharti na vigezo’ pekee, badala yake kila sharti na kigezo lifahamike…

Read More

Samia ateua mrithi wa Mafuru

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investiment (WHi), Dk Fred Msemwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango. Taarifa ya kuteuliwa kwake imetolewa leo, Februari 27, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Sharifa Nyanga….

Read More

Aliyeua wezi kwa kuwakata mapanga, ahukumiwa kunyongwa

Arusha. Madhara ya kuchukua Sheria mkononi. Ndicho kilichomkuta mkazi wa Mara, Rhobi Chacha, ambaye amekwaa kisiki Mahakama ya Rufani iliyobariki adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa kuwauwa watu wawili waliotuhumiwa kwa wizi. Tukio hilo lilitokea Aprili 28,2018 katika Kijiji cha Nyarwana wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, kundi la watu karibu 50 akiwemo Chacha wakiwa na…

Read More

Kiharusi sasa tishio, mbinu za kukiepuka

Dar es Salaam. Ongezeko la wagonjwa wa kiharusi nchini, limewaibua wataalamu wa afya wanaotaja mambo ya kuepuka kupata tatizo hilo, huku wenye shinikizo la juu la damu wakitajwa kuwa hatarini zaidi. Matumizi yasiyo sahihi ya dawa za kisukari, shinikizo la juu la damu lisilotibiwa, matumizi ya dawa za kulevya, unywaji dawa bila ushauri wa daktari,…

Read More