
Kwa mkwamo huu, mnaonaje Katiba mpya ikaandikwa na wasomi?
Ni ukweli ulio dhahiri kuwa Tanzania tuko katika mkwamo wa safari ya kuandika Katiba mpya na ukichunguza sana utabaini maslahi ya kisiasa ndio kizingiti cha mchakato huu, ndio maana nauliza, mnaonaje Katibampya ikiandikwa na wasomi? Nasema hivyo kwa sababu ukichunguza mkwamo tulio nao, kwa sehemu kubwa unatokana na wahafidhina (conservatives) ndani ya Chama cha Mapinduzi…