
Marufuku shughuli za kibinadamu mapango ya Amboni
Tanga. Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha amepiga marufuku shughuli zote za kibinadamu zinazofanyika katika Hifadhi ya Mapango ya Amboni, kama vile kukata miti, kuchimba mchanga, kwani kufanya hivyo kunaweza kuharibu uhalisia wa eneo hilo. Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya kutangaza vivutio vya utalii kwa Mkoa wa Tanga iliyofanyika katika mapango hayo…