ACT Wazalendo yatoa neno uendeshaji bandari ya Malindi

Unguja. Chama cha ACT-Wazalendo kimeitaka Serikali kuvunja mkataba na mwekezaji anayeendesha Bandari ya Malindi na kurudisha shughuli za uendeshaji wa bandari kwa Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC). Chama hicho kimedai mwekezaji huyo aliyekuwepo imeshindwa kuweka ufanisi wa bandari hali inayosababisha usumbufu kwa watumiaji, imezorotesha biashara na kuongeza gharama za maisha kwa wananchi wa Zanzibar inayotokana…

Read More

Wataalamu wa lishe wataka baraza la kitaaluma

Dar es Salaam. Wataalamu wa lishe nchini Tanzania wamesema licha ya umuhimu wao katika jamii, bado hawatambuliki rasmi kama sehemu ya kada ya afya, jambo linalosababisha wapate malipo duni katika utendaji wao. Pia wamesema hakuna bodi maalumu inayosimamia utendaji wa wanataaluma wa lishe nchini, hali inayosababisha watu wasio na taaluma hiyo kufanya kazi kama wataalamu…

Read More

Tanzania yaja na sera mpya ya uchumi wa buluu

Dar es Salaam. Ili kuhakikisha sekta ya uchumi wa buluu inagusa maisha ya watu kwa vitendo, Serikali imeanzisha sera mpya ya uchumi wa buluu nchini iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais. Sera hiyo imeanzishwa ili kuhakikisha sekta hiyo mpya ambayo ndiyo uelekeo wa nchi nyingi inaongozwa kwa utaratibu wa kisera na sheria. Hayo…

Read More

Mtoto mwenye ulemavu ashambuliwa na panya watatu hadi kufa

Morogoro. Mtoto mwenye ulemavu wa akili na viungo, Christian Ngalika (Dotto) mwenye umri wa miaka 12 amefariki dunia baada ya kushambuliwa na panya watatu sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa nyumbani kwao Kata ya Mang’ula Wilaya ya Kilombero. Akisimulia tukio hilo babu wa mtoto huyo, Salumu Natechi amesema limetokea jana Februari 26, 2025 wakati mama…

Read More

Nyaya chini ya bahari kuimarisha matumizi ya kidigitali Zanzibar

Unguja, Zanzibar. Vodacom Tanzania PLC imetiliana saini makubaliano ya kimkakati na Shirika la Miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA), ili kuboresha huduma za mawasiliano na kuharakisha mabadiliko ya kidijitali visiwani Zanzibar. Mkataba huo, umesainiwa leo Alhamis 27, 2025 katika ofisi za Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, unairuhusu Vodacom kutumia miundombinu…

Read More

Milioni 400 za bodaboda Arusha bado kizungumkuti

Arusha. Sakata la ‘upigaji’ wa Sh400 milioni zinazodaiwa kuchotwa kwenye akaunti ya Umoja wa Bodaboda Mkoa wa Arusha (Uboma), limeingia sura mpya baada ya viongozi wa umoja huo kuililia Serikali iingilie kati ili fedha hizo zipatikane na kuimarisha mfuko wao na kuwasaidia kukua kiuchumi. Kati ya fedha hizo Sh280 milioni zinadaiwa kuchotwa benki kwa nyakati…

Read More

Vuguvugu la wasio na ajira lawashtua, wadau waonya

Dar es Salaam. Siku nne baada ya kukamatwa kwa viongozi wa Umoja cha Walimu Wasiokuwa na ajira Tanzania (Neto) kwa kile kilichoelezwa umoja huo haujasajiliwa, wadau wameitaka Serikali kutafuta suluhisho la kukabiliana na ukosefu wa ajira badala ya kushughulika na watu wanaopaza sauti kuhusu changamoto hiyo. Sintofahamu hii  ilianza Februari 21, walipoibuka viongozi wa umoja…

Read More

Serikali yaanika mkakati kupunguza bei ya gesi

Muheza. Huenda kilio cha bei ya gesi nchini kikapata suluhu baada ya Serikali kuweka wazi mikakati yake ya kuhakikisha inawapunguzia wananchi gharama ya nishati hiyo. Mikakati hiyo kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan ni pamoja na kutoa ruzuku kwa wanaochakata gesi kuwa nishati na kuweka mazingira rafiki yatakayochochea ushiriki wa sekta binafsi kwenye shughuli…

Read More