
Watatu waliofariki kwa ajali Kimara watambuliwa, yumo kondakta wa daladala
Dar es Salaam. Miili ya watu watatu kati ya wanne waliyofariki katika ajali iliyohusisha lori lililohama njia na kuparamia kituo cha bodaboda kilichopo Kimara Stop Over jijini Dar es Salaam imetambuliwa, huku mmoja ikielezwa alikuwa ni kondakta wa daladala. Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana Februari 14, 2025 ambapo lori hilo lilikuwa likitokea Morogoro…