
Mkutano wa viongozi M23 wavurugika, milipuko yasikika Bukavu DRC
Bukavu. Watu kadhaa wanahofiwa kujeruhiwa baada ya milipuko miwili kutokea wakati wa mkutano wa viongozi wa kundi la waasi la M23 katika mji wa Bukavu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Picha na video zilizosambazwa mitandaoni leo, Alhamisi Februari 27, 2025, zinaonyesha taharuki huku watu wakikimbia kwa hofu, na miili ikiwa imetapakaa damu….