Aliyemezwa na nyangumi atapikwa akiwa hai, asimulia kilichomkuta
Mwanza. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Dell Simancas amerekodi tukio la mwanaye, Adrian Simancas (24) akimezwa na samaki aina ya Nyangumi mwenye nundu kisha kutapikwa akiwa hai. CNN imeripoti kuwa tukio hilo la kushtua limetokea Jumamosi Februari 8, 2025, wakati Adrian na baba yake walipokuwa wakipiga kasia kila mmoja kwenye boti yake inachoelea majini (Kayaker)…