Mambo yanayomsubiri kamishna mpya ZRA
Unguja. Wakati Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Said Kiondo Athumani akikabidhiwa mikoba rasmi kuendesha taasisi hiyo, mambo kadhaa yanamsubiri ikiwamo kuzungumza na wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari. Pia, anapaswa kuweka mikakati kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa risiti za kielektroniki kwa kuwa, wengi wanatajwa kukwepa jukumu hilo kwa kisingizo cha mashine kukosa mtandao. Kiondo anachukua…