CAG Kichere ayang’ata sikio mashirika ya umma
Kibaha. Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG), Charles Kichere amesema mkakati wa serikali kwa sasa ni kuona mashirika ya umma nchini yanajiimarisha kiuchumi ili yajiendeshe bila kutegemea ruzuku ya serikali. Amesema mbali na kujitegemea, pia mashirika hayo yanapaswa kujiwekea utaratibu wa kupeleka gawio la faida yatakayokuwa yanazalisha serikalini kila mwaka, hali itakayosaidia kukuza uchumi…