ACT Wazalendo yaunda kamati kuandaa Ilani ya Uchaguzi 2025
Dar es Salaam. Kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu amefanya uteuzi wa kamati ya kuandika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025 ya chama hicho itakayokwenda kuuzwa kwa wananchi. ACT Wazalendo kimekuwa chama cha kwanza nchini kuanzisha michakato ya uchaguzi mapema na tayari kimefungua dirisha kwa wanachama wake wenye nia…