Sura mbili wananchi waliowekeza pesa zao LBL, mchumi aonya

Dar es Salaam. Wakati baadhi ya watu wakiwekeza fedha kwenye kampuni za upatu, imeelezwa kuwa, ukuaji wa teknolojia unakuja na fursa nyingi, hivyo kuzijua halali na zisizo halali inachukua muda, huku wengine wakijikuta wanatapeliwa. Akizungumzia hilo leo Jumatano Februari 26, 2025  mchumi Profesa Haji Semboja amesema, “tatizo kubwa hadi mtu kutapeliwa ni kutokana na elimu…

Read More

Majaliwa ataka viongozi wa dini kukemea mmomonyoko wa maadili

Arusha. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa dini nchini kuendelea kukemea vitendo vinavyochangia mmomonyoko wa maadili, kama vile matumizi ya dawa za kulevya. Majaliwa amesema hayo leo, Februari 26, 2025, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Maridhiano Kitaifa (Maridhiano Day) yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Akizungumza kwa…

Read More

INEC mguu sawa kugawa majimbo, wadau waonyesha njia

Moro/Dar.  Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuanza mchakato wa kuchunguza na kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi , hatua ambayo imewaibua wadau wakionyesha njia sahihi ya kufikia lengo hilo. Katika maandalizi hayo, Inec imesema itaanza kupokea mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali kuanzia kesho Februari 27 hadi Machi 26, mwaka huu….

Read More

Ajali ziara ya CCM Mbeya, miili kuagwa kesho

Mbeya. Wakati miili ya marehemu waliofariki kwa ajali jana kwenye ziara ya chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya, majeruhi wazungumzia maendeleo ya afya zao. Jana Jumanne Februari 25, 2025 watu watatu walifariki papo hapo baada ya gari la serikali walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la Kampuni ya CRN katika eneo la Shamwengo…

Read More

Raia wa Burundi aliyeua akiwa amelewa atupwa jela

Kigoma. Uamuzi wa raia wa Burundi, Isaka Erick (20) kukiri kosa la kuua bila kukusudia, umemuokoa na adhabu ya kifo iwapo ingethibitishwa alilitenda kwa kukusudia na akatiwa hatiani. Kwa mujibu wa kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022, mtu yeyote ambaye kwa dhamira ya uovu anasababisha kifo cha mtu mwingine…

Read More

Tanzania mbioni matibabu, upasuaji kwa roboti

Dar es Salaam. Tanzania inakaribia kuingia katika teknolojia ya upasuaji kwa kutumia akili mnemba ‘roboti’ baada ya baadhi ya hospitali nchini kuanza maandalizi ya huduma hiyo kwa kutoa mafunzo kwa wataalamu. Hospitali hizo ni pamoja na Taasisi ya Saratani Ocean Road ORCI, Hospitali ya Benjamin Mkapa BMH na Hospitali ya Saifee Tanzania. Desemba 31, 2024…

Read More

Aliyebeba kibuyu tukio la Muungano azikwa, Shoo ataka umakini kwenye elimu

Hai. Wakati Sifael Shuma (92)aliyekuwa mmoja wa vijana wanne walioshiriki tukio la kuchanganya udongo, Aprili 26,1965,akizikwa nyumbani kwake Machame, Wilaya ya Hai, Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo ameiomba Serikali kuwekeza katika sekta ya elimu na kuhakikisha wanazalishwa vijana wenye elimu bora.  Dk Shoo amesema…

Read More