
Wafanyabiashara wa Kariakoo waanza kuchukua fomu za kurejea sokoni
Dar es Salaam. Mamia ya wafanyabiashara waliokidhi vigezo vya kurejea soko la Kariakoo wamejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuanza tena biashara sokoni hapo, huku baadhi yao wakitaja changamoto ya kutojua kodi wanayotakiwa kulipa. Hatua ya kurejeshwa kwa wafanyabiashara hao inakuja baada ya kukamilika kwa ukarabati wa soko hilo lililoungua Julai 10, 2021 na kuteketeza…