
HADITHI: Bomu Mkononi – 21
“HAYO ni maneno ya kunishutumu mke wangu lakini kama unanifikiria hivyo sawa.” “Na mimi nakwambia sawa.” Ukawa mwisho wa maneno yetu. Hata hivyo, usiku ule nilijidai kukasirika, kila mmoja akalala ubavu wake. Asubuhi kulipokucha mimi ndiye niliyeanza kumsemesha, nikajifanya yale ya jana sikuwa nayo tena. Lakini moyoni mwangu nilikuwa nayo kwamba mume wangu pia hakuwa…