
Simba yaishusha Yanga kileleni, yaifumua Tabora United
NYUKI wa Tabora leo wametulizwa nyumbani baada ya kufumuliwa tena mabao 3-0 na Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara na kuhitimisha tambo ilizokuwa nazo timu hiyo mbele ya vigogo, ikithibitisha unyonge uliopitiliza dhidi ya Mnyama kwa kufungwa jumla ya mabao 12-0 katika mechi nne walizokutana katika ligi kuanzia msimu uliopita. Tabora ilionekana tishio baada…