
Wanafunzi saba wafukuzwa shule Geita, wengine 64 wasimamishwa
Geita. Bodi ya Shule ya Sekondari Geita imewafukuza shule wanafunzi saba na kuwasimamisha kwa vipindi tofauti wanafunzi wengine 64 wa kidato cha sita, baada ya kubainika kushiriki kwenye vurugu zilizotokea shuleni hapo Februari 20, 2025 na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh2.9 milioni. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi leo Februari 24,…