
Lissu ataja masharti kina Mdee kurejea Chadema
Dar es Salaam. Wakati baadhi ya wabunge 19 wa viti maalumu waliofukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiendelea na harakati za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu amebainisha kile kinachopaswa kufanywa iwapo wanataka kurejea. Lissu amesema Halima Mdee na wenzake 18 ambao walivuliwa uanachama Novemba 27,…