
Beki Namungo kadi nyekundu, refa aliyemlima kimakosa akaushiwa
BEKI wa kati wa Namungo, Derrick Mukombozi amefutiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyopewa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba uliopigwa Februari 19 kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi na wenyeji kupoteza kwa mabao 3-0. Mukombozi alipewa kadi hiyo nyekundu iliyozua utata na mwamuzi Japhet Smarti kutoka Katavi dakika ya…