
ADC yatofautiana na Chadema, yaja na ‘Kama Mbwai na Iwe Mbwai’
Mwanza. “Kama Mbwai na Iwe Mbwai”. Hii ndiyo kauli anayoitumia Mwenyekiti wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Taifa, Shaban Itutu kuelezea msimamo wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025. Itutu ametoa kauli hiyo baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuja na kaulimbiu yake ya ‘No Reform, No Election’…