Kauli ya Sheikh Ponda kwenye maziko ya Sheikh Muwinge

Morogoro. Waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kwa ujumla wametakiwa kuishi wakiwa na jukumu la kuhakikisha wanaacha alama njema duniani kwa kuwa, maisha ya mwanadamu ni safari fupi. Wito huo umetolewa leo Jumatano, Februari 19, 2025 na Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu, Sheikh Issa Ponda wakati akizungumza kabla ya mazishi ya mwanazuoni mkongwe…

Read More

Fursa, changamoto dhahabu ikifikia bei ya juu zaidi

Dar es Salaam. Bei ya dhahabu imepanda na kufikia rekodi ya Sh7.5 milioni kwa wakia moja (troy ounce) mnamo Februari 15, 2025, ikiwa ndio kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa, kwa mujibu wa viwango vya ubadilishaji wa fedha vya Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Ongezeko hilo la Sh1.3 milioni kutoka wastani wa Sh6.2 milioni mnamo…

Read More

Mahakama yatupa maombi ya watumishi wa zamani wa Takukuru

Dodoma. Wafanyakazi wa zamani wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waliokuwa wamefungua shauri kuomba mapitio ya mahakama, wakipinga kufutwa kwao kazi, wamekwaa kisiki baada ya maombi yao kutupwa. Watumishi hao wa zamani wa Takukuru, Hassan Chamshama, Hamis Mkao na Ibrahim Liban, walifungua maombi namba 27443/2024 dhidi ya mwenyekiti wa kamati ya usimamizi…

Read More

Anayedaiwa kuwachapa fimbo wanafunzi wa madrasa kortini

Dar es Salaam. Mwalimu wa Madrasa, Musa Bashiru Musa (24) ambaye kipande cha picha jongefu (video) kilisambaa katika mitandao ya kijamii kikimuonyesha akiwapiga fimbo za mikononi wanafunzi wake, amepandishwa kizimbani kujibu tuhuma zake. Musa ambaye ni mkazi wa Mbagala Kiburugwa, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke na kusomewa mashtaka mawili ya kuwafanyia ukatili watoto…

Read More

Kocha wa Diarra avunja mkataba Yanga, sababu yatajwa

WAKATI hali ikiwa si shwari kwa kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra kutokana na kufungwa mabao mepesi hivi karibuni yanayoonekana yanatokana na makosa binafsi, kocha aliyekuwa akimnoa ndani ya timu hiyo ameomba kuondoka na taarifa zinasema tayari ametoa FAR Rabat ya Morocco. Kocha huyo anayemnoa Diarra na makipa wengine katika kikosi cha Yanga, alikuwa…

Read More

Shirika la Mazingira la UN linataka hatua za haraka juu ya 'shida ya sayari tatu' – maswala ya ulimwengu

“Mwaka jana ilileta mafanikio na tamaa katika juhudi za ulimwengu za kukabiliana na shida ya sayari tatu,” AlisemaUnep Mkurugenzi Mtendaji Inger Andersen, akianzisha hivi karibuni ya shirika hilo Ripoti ya kila mwaka. Alionyesha pia mvutano unaoendelea wa kijiografia ambao unazuia ushirikiano wa mazingira. “Multilateralism ya mazingira wakati mwingine ni mbaya na ngumu. Lakini hata katika…

Read More