Watu sita wamefariki dunia na wengine 49 wamejeruhiwa baada ya ajali kutokea eneo la Chigongwe, Dodoma, usiku wa Machi 3, 2025.
Ajali hiyo ilihusisha basi la AN Classic lenye namba za usajili T405 BYS, lililokuwa likielekea Kigoma, na lori lililoharibika barabarani bila alama za tahadhari. Mashuhuda wamesema mwendokasi wa basi huenda ulichangia ajali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, alifika eneo la tukio na kusema kuwa majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, ambapo 23 tayari wamefanyiwa upasuaji. Miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini kusubiri utambuzi wa ndugu zao.