Magari yagongana Moro, wawili wafariki

Morogoro. Watu wawili wamethibitika kufariki dunia papohapo katika tukio la ajiali lililohusisha magari mawili kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la nanenane Manispaa ya Morogoro barabara kuu ya Morogoro Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea saa saba usiku wa kuamkia leo Machi 04, 2025. Magari hayo mawili moja ni lori la mafuta likiwa linatokea uelekeo wa Dar es Salaam likiwa na tela mbili za mafuta  huku gari lingine likiwa ni lori la mizigo likiwa linatokea uelekeo wa Msamvu kuelekea Dar es Salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Faraja Pazzy amesema hadi sasa idadi kamili ya watu waliofariki bado haijafahamika wanaendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo ili kubaini madhara zaidi.

Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo akiwamo Juma Ramadhan amesema, “gari mbili fuso zilikuwa zinatoka uelekeo wa Msamvu zikiwa zimeongozana walivyofika kwenye tuta yule wa mbele alifunga breki kwa ajili ya tuta sasa yule wa nyuma baada ya kuona mwenzake kafunga breki alijaribu kumkwepa ndiyo akagongana uso kwa uso na hilo lori la mafuta”, Amesema Juma Ramadhan.

Related Posts