
‘Ziara bosi wa Unesco kuiletea neema Tanzania’
Unguja. Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), Audrey Azoulay imetajwa kuleta neema Tanzania kwa shirika hilo kuongeza utaalamu na msaada wa kifedha kusaidia maeneo ya urithi wa dunia. Tangu Machi mosi, Mkurugenzi huyo amefanya ziara Tanzania bara na Zanzibar kwa kukutana na viongozi wakuu wa nchi…