Huzuni kubwa imetanda katika familia ya Hassan, mkazi wa Temeke, baada ya watoto wake wawili kupoteza maisha katika ajali mbaya eneo la Uhasibu. Watoto hao walitoka nyumbani wakisema wanakwenda shule, lakini badala yake walielekea kwa bibi yao.
Familia iliwatafuta kwa siku mbili bila mafanikio, hadi taarifa za polisi zilipoeleza kuwa miili ya watoto wawili waliopoteza maisha katika ajali ilikuwa imepokelewa na jeshi la polisi.
Msikilize Mama mzazi wa watoto hao alivyofunguka kwa uchungu.