Shigongo Awataka vijana Kufanya Kazi, Acheni Kunywa Pombe Hovyo – Global Publishers



Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, amewataka vijana wa Buchosa kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia maendeleo, huku akiwaasa kuachana na unywaji wa pombe kupitiliza ambao hauna faida kwao.

Ameyasema hayo alipokuwa katika Kijiji cha Isaka, Kata ya Nyehunge, Jimbo la Buchosa.

Amesema vijana wengi wa Buchosa wamekumbwa na tatizo la unywaji wa pombe kupitiliza ambao hauna faida na unadidimiza maisha yao.

Sambamba na hayo, amewataka wananchi wa Buchosa kufuata sheria na taratibu za nchi zinavyotaka.











Related Posts