
AKILI ZA KIJIWENI: Minziro, Ahmad Ally wajihadhari
MSIMU huu umekuwa na upepo ambao sio mzuri kwa makocha na hadi hapa akili za kijiweni zinapochakata kuna makocha kama 14 hivi wameondoka kwenye timu zao kwa kufungishwa virago. Ni makocha wawili tu ambao wameondoka kwa uamuzi wao binafsi na sio kwa sababu ya matokeo yasiyoridhisha ambao ni Abdi Moalin na Sead Ramovic walioziacha timu…