
Safari ya benki ilivyomuacha na ulemavu wa kudumu mwalimu
Mufindi. Aprili 21, 2019 inabaki kwenye kumbukumbu za mwalimu Silvester Lyuvale, siku aliyopata ajali iliyomsababishia ulemavu wa kudumu. Lyuvale (52), mwalimu wa Shule ya Msingi Kinyanambo katika Halmashauri ya Mji Mafinga, wilayani Mufindi, mkoani Iringa baada ya ajali alikatwa miguu yote miwili. Alipopata ajali hiyo alikuwa Ofisa Elimu Kata ya Wambi. Akizungumza na Mwananchi, anasema…