
135,027 waomba ajira TRA, kuajiriwa kabla ya Juni
Dodoma. Watu 135,027 wameomba ajira katika nafasi 1,596 zilizotangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Februari 6, mwaka 2025 TRA ilitangaza nafasi za ajira katika idara za mapato ya ndani, forodha na ushuru, usimamizi na utawala wa raslimali watu. Nyingine ni utafiti na mipango, fedha, ukaguzi wa ndani, mambo ya ndani na idara ya viatarishi…