
Kijana atoweka kwa siku 10, mama yake apaza sauti
Geita. Abrahaman Habiye, mkazi wa Mtaa wa Uwanja, Kata ya Nyankumbu mjini Geita anadaiwa kutoweka tangu Machi Mosi, 2025 alipochukuliwa na watu wasiojulikana. Habiye (24), aliyekuwa akiuza duka la nguo la mama yake, inadaiwa alifuatwa na watu walioshuka kwenye gari jeupe aina ya Toyota Land Cruiser lenye vioo vyeusi waliojifanya wateja. Jeshi la Polisi limethibitisha…