Adakwa kwa kuanzisha kituo feki cha polisi

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Collins Leitich mkazi wa Kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya anashikiliwa na polisi nchini humo kwa kosa la kuanzisha kituo cha polisi na kukiendesha kinyemela bila ya idhini ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS). Kwa mujibu wa mtandao wa Tuko wa nchini humo, Leitich alipaka kituo hicho rangi…

Read More

Kinachofanyika udhibiti athari za tumbaku Tanzania

Dar es Salaam. Wakati kila mwaka watu 21,800 wakipoteza maisha nchini kwa maradhi yatokanayo na uvutaji wa tumbaku, Serikali imeeleza hatua zinazochukuliwa kudhibiti athari za zao hilo. Kwa mujibu wa taarifa za uwekezaji na udhibiti wa tumbaku Tanzania (Investment Case for Tobacco Control in Tanzania), kila mwaka vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku huchangia asilimia…

Read More

Winga Mrundi kumng’oa Adebayor Singida

SINGIDA Black Stars inapiga hesabu kali za kumbeba winga wa Al Hilal, Jean Claude Girumugisha ili atue katika kikosi hicho kuchukua nafasi ya Victor Adebayor waliye mbioni kumsitishia mkataba alionao mwishoni mwa msimu huu. Adebayor aliyeanza kuitumikia timu hiyo mara dirisha dogo la usajili lilipofunguliwa Desemba mwaka jana, ameshindwa kuonyesha makeke wala kupenya katika kikosi…

Read More

Aziz KI, Nouma watemwa Burkina Faso

KIUNGO mshambuliaji nyota wa Yanga, Stephane Aziz Ki na beki wa kushoto wa Simba, Valentino Nouma wametemwa katika kikosi cha Burkina Faso kilichotangazwa kuitwa leo Jumatatu na kocha Brama Traore kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 Burkina Faso itakuwa nyumbani Machi 16 2025 kucheza mchezo wa tano…

Read More

Wawili wakutwa na maambukizi ya Mpox Tanzania    

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imesema imewabaini watu wawili kuwa na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Mpox. Hii ni mara ya kwanza ugonjwa wa Mpox kuingia nchini. Taarifa hiyo inakuja siku tatu tangu picha mjongeo iliyosambaa katika makundi ya sogozi, ikionyesha watu wawili wakiwa wamejirekodi na kudai kuwa na…

Read More

Tuwalee wanafunzi kwa hoja si kwa viboko

Katika gazeti hili toleo la tarehe 5/3/2025 kulikuwa na kichwa cha habari: “Mwanafunzi afariki dunia kwa kipigo.”  Halafu katika tolea la tarehe 6/3/2025, mhariri akaandika maoni ya gazeti  kwa kichwa cha habari kisemacho: “Viboko hadi kifo vikomeshwe shuleni.”  Nampongeza mhariri kwa maoni hayo mazuri. Na kesho yake tarehe 7/3/2025 tukaona tena habari hii: “Sababu mwili…

Read More

Wataka kibano walimu wanaoendekeza viboko

Simiyu. Serikali imeshauriwa kuwaondoa katika nafasi zao walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari, watakaoshindwa kusimamia utaratibu,kanuni na miongozo ya utoaji wa adhabu ya viboko kwa wanafunzi katika shule zao na kusababisha madhara kwa wanafunzi. Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,  ilitoa Waraka wa Elimu Na.24 kuhusu adhabu…

Read More

Kinachojadiliwa Kamati Kuu Chadema hiki hapa

Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inakutana katika kikao maalumu kikiwa na ajenda mbalimbali, ikiwemo uteuzi wa wakurugenzi, makatibu wa kanda, na taarifa ya utekelezaji wa ‘No Reforms No Election’. Ajenda hizo zimeanza kujadiliwa katika kikao hicho kilichoanza leo Jumatatu, Machi 10, 2025 na kinatarajiwa kuhitimishwa kesho Jumanne, makao…

Read More