
Butiku amwelezea Profesa Sarungi, kuagwa Karimjee Dar
Dar es Salaam. Waombolezaji wameendelea kufika nyumbani kwa Profesa Philemon Sarungi kutoa pole akiwemo Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, ambaye amesema Profesa Sarungi, alikuwa mtu mwadilifu na aliyependa nchi yake. Profesa Sarungi ambaye amewahi kuhudumu kama waziri wa wizara mbalimbali na mbunge wa zamani wa jimbo la Rorya alifariki Machi 5, 2025…