
IGP Wambura: Hatutakubali amani ivurugwe kwa kisingizio cha uchaguzi
Moshi. Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillus Wambura amesema jeshi hilo halitakubali mtu yeyote, kwa sababu yoyote, avuruge amani ya nchi kwa kisingizio cha harakati za uchaguzi. IGP Wambura ameyasema hayo leo Ijumaa Machi 7, 2025, wakati wa kufunga mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi kwa ngazi ya Sajini na Koplo,…