
Bomoa bomoa nyingine yaja, maeneo 111 kupangwa upya
Dodoma. Maeneo 111 katika mikoa 24 yenye makazi duni na yanayoendelezwa kiholela nchini, yanaanza kufanyiwa maboresho kupitia upangaji upya wa miji, huku Serikali ikiahidi kushirikisha wananchi kwa karibu katika mchakato huo. Hatua hiyo inatekelezwa chini ya Programu ya Uendelezaji wa Miji, inayoendeshwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Marekebisho hayo yanachochewa na…