
Aliyebuni jina ‘Tanzania’ afariki dunia
Dar es Salaam. Mohammed Iqbal Dar mbunifu wa jina la Tanzania, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 jijini Birmingham, Uingereza, ambako aliishi tangu ahamie mwaka 1965. Kifo chake kimetokea baada ya kuugua kwa muda wa miaka takriban 10, ambapo alikuwa hawezi kutembea akiwa chini ya uangalizi wa karibu nyumbani. Mohammed Iqbal Dar alizaliwa…